*Awataka viongozi wa vyama vya ushirika wawe waaminifu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasimali za vyama hivyo na kwamba Serikali haitalipa deni lolote lililokopwa na vyama hivyo.
“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya awamu ya tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhilifu huo.”

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku wafanyabiashara kuwaibia wakulima kwa kununua kahawa mbichi ikiwa shambani maarufu kama butura.Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara pamoja na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Waziri Mkuu amesema Serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao si waaminifu na wabadhilifu wa mali za ushirika.”Tunahitaji wakulima wapate fedha.”Amesema Serikali itahakikisha wafanyabiashara wote, hususani wa mazao ya kilimo wanakuwa na mfumo sahihi wa ununuzi wa mazao utakao ongeza tija kwao na kwa wakulima.

Amesema kwa sasa Serikali inataka kuondoa mfumo uliopo wa vyama vya ushirika kufanya biashara na badala yake jukumu hilo libakie kwa wafanyabiashara.Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao waihakikishie Serikali kwamba watanunua kahawa yote iliyopo kwa wakulima pamoja na kwenye vyama vya ushirika. Wafanyabiashara wameridhia kununua kahawa yote.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, wanne kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijhage na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma bango lenye malalamiko ya mmoja wa wananchi wa Bukoba wakati alipowasalimia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne mkoani humo, Oktoba , 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti na kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Baadhi ya wafanyabiashara wa zao la kahawa wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...