KAMPUNI ya Taxify imezindua huduma ya Taxify Boda jijini Dar es salaam na huduma hii sasa itakuwa inapatikana katika jiji la Dar es salaam na Mwanza. 

Huduma hii inawezesha watanzania kupata usafiri wa bodaboda kwa kutumia teknologia ya Taxify App inayopatikana katika simu ya kiganja kwa urahisi na bei nafuu na


Tanzania inakuwa nchi ya tatu ambapo huduma hiii imezinduliwa.


 Meneja Mkuu Afrika Mashariki wa Taxify, 
Shivachi Muleji 
 
alisema kuwa kampuni ilibuni huduma hii ya Taxify Boda kutokana na kuongezeko kwa uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika wa pikipiki.

"Tatizo la foleni Dar es salaam umechochea ukuaji wa uhitaji wa usafiri wa pikipiki katika jiji la Dar es salaam, na uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika ni mojawapo ya kipaumbele kwa wasafarishaji na huduma yetu inatoa suluhisho kwa changamoto hizi” alisema 

 Meneja Mkuu Tanzania, Remmy Eseka, 
alisema kuwa huduma ya Taxify Boda imejikita katika kuhakikisha usalama wa madereva na abiria, na madereva wote ambao wamejisajili na huduma yetu wameelimishwa kuhusiana na hili.

“Teknologia yetu inatuwezesha kufuatilia tabia ya madereva na huwezesha abiria uwezo wa kutoa maoni kuhusu huduma za dereva na safari yake kila anapotumia huduma zetu”

Kampuni imeweka mwongozo mkamilifu wa kuhakikisha usalama wa abiria. Wateja na madereva watahitajika kuvaa kofia ngumu na jaketi ya reflecta na tabia ya wateja kukaa upande ni marufuku kwa wateja na kuruhusiwa tu, kwa mteja aliye na ulemavu. 

Pia, kuhakikisha usalama zaidi kwa wateja na madereva, kampuni inafutiliwa ushirkiano na makmpuni mbalimbali inayotoa huduma ya kwanza baada ya ajali na makampuni ambayo yanaweza kutoa usaidizi kwa dereva au abiria wakati wa dharura au ajali. 

Kampuni imewekeza pia na mafunzo ziada ya udereva na huduma ya kwanza na kutoa vyeti kwa wote waliojisajili na huduma. “Tunatamani kupunguza pengo la ufanisi wa madereva kwa kutoa mafundisho na vyeti vya ubora,” alisema Eseka. Pia kampuni itashirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutelekeza miongozo ya usalama. 

Aidha, Eseka alielezea kuwa huduma yao itasaidia madereva bodaboda kujiendeleza kila moja na maendeleo ya kibinafsi kutokana na mfumo wao wa biashara. "Tunataka kusaidia madereva wa pikipiki kufanya biashara zao kwa njia ya kitaaluma zaidi kwa kutoa jukwaa la kufuatilia safari, mapato na hata kupanga mipango ya maendeleo ya kibinafsi kama kujiunga na SACCO. Kwa kuwa sasa hivi madereva boda boda wanajitahidi kuanzisha makundi rasmi, Taxify Boda itatoa elimu kwa vikundi na hatimaye elimu itawasadia kuleta maendeleo kama kununua pipipiki,” alisema.

Eseka alielezea kuwa utoaji wa huduma ya teknologia inayounganisha abiria na madereva boda boda ni njia moja kampuni inachangia kuboresha muundo wa uchumi wa usafirishaji usio rasmi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...