Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Benki ya Amana imetimiza miaka mitatu ya kufanya biashara na kutimiza ndoto ya watanzania kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo mbalimbali wakishirikiana na Kampuni ya Property International (PIL).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.

Rajab amesema kuwa, Katika mkopo huo watu wengi wameweza kunufaika kutumia viwanja hivyo kupata mkopo kupitia benki hiyo ili  kuwezesha kuinua uchumi na kukuza biashara zao."Mteja anatakiwa atangulize asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kulipa kiasi kilichobaki kwa muda uziodi mwaka mmoja na nusu ila kwa sasa tumeongeza hadi miaka mitatu,"amesema Rajab.

Amesema, kutokana na kuwajali wateja wao wameongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kuwapunguzia faida toka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka mmoja.
 Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano wa Benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wateja wa benki ya Amana Stephano Matesi akipokea hati ya kiwanja kutoka kwa  Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab leo kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano kati ya benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL) 
Picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...