Na Rhoda James - Geita

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza mgodi wa Nyati Resources ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita kutolipa gawio Serikali ya kijiji cha Ngula kuanzia tarehe 2 Novemba, 2018 ili kutoa nafasi ya uchunguzi kujua ni nani mmiliki halisi wa eneo hilo la mgodi.

Ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 2 hadi 3 Novemba, 2018 iliyolenga kukagua machimbo ya madini katika Mkoa wa Geita.

Pamoja na ukaguzi huo, Biteko ameeleza kuwa, ametembelea machimbo hayo ili kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina ya Kijiji cha Ngula na mkazi wa kijiji hicho Mindi Masasi. 

 Akizungumza katika kikao hicho, Biteko ameutaka Mgodi huo wa Nyati Resources ltd kutolipa gawio kwa kijiji hicho kwa kuwa kuna malalamiko kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho ambaye ni Mindi Masasi.

Biteko ameeleza kuwa mgodi huo umeanza uzalishaji tangu Desemba, 2017 na umekuwa ukimlipa Mindi Masasi gawio kwa zaidi ya mwaka kwa kuwa wakati wanaanza uzalishaji wa dhahabu wamemkuta katika ardhi hiyo ambayo amekuwa akiishi tangu mwaka 1954 lakini sasa kijiji kinadai kuwa ardhi hiyo ni mali yao na wao ndio wenye haki ya kulipwa gawio hiyo. 
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akihutubia wananchi wa kijiji cha Ngula na wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa Nyati Resources Ltd (hawapo pichani) katika mkoa wa Geita tarehe 2 Novemba, 2018


Mkazi wa kijiji cha Ngula, Mindi Masasi (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani). Katikati ni Mtoto wa Mindi Masasi, Makanika Chalo pamoja na Mwenyekiti wa kata ya Bujula (jina halikupatikana)
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngula mara baada ya kukagua Mgodi wa Nyati Resources Ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...