Na Mwandishi wetu
MKUU wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wasichana kutumia fursa za uwapo wa Tehama kutimiza ndoto zao.
Ushauri huo aliutoa mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza na wasichana wa sekondari waliokuwa katika jukwaa la ujasiriamali kwa wasichana.
Jumla ya wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam walijumuika kwa siku mbili katika jukwaa ambapo miradi yao iliyobuniwa kwa kutumia teknolojia ilifanyiwa uhakiki na mshindi kupewa tuzo.
Katika jukwaa hilo lililoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Apps and Girls likishirikiana na Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Jokate Mwegelo alisema wasichana wa nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko katika maisha yao na jamii zao wanachotakiwa ni kutumia fursa zilizopo vizuri.
Alisema mafunzo ambayo wasichana hao wameyachukua ni fursa nzuri ya kujibadilisha na kusema hawana sababu ya kuwa waoga katika hilo bali wajitume inavyostahili.
Alisema katika utekelezaji wa ndoto zao kunakuwa na vikwazo vingi lakini ni wajibu wao kuvishinda na kusonga mbele.
Alitolea mfano yeye ambapo baada ya kusoma alisimama kidogo na kuwaambia wazazi wake kwamba anasimama kidogo ili atengeneze bidhaa ambazo zingeweza kumfanya kutimiza ndoto yake.
Alisema japokuwa wazazi wake hawakumwelewa alikazania alichofikiri na ndio chanzo cha kidoti, alama inayotambuliwa na watu wengi.
Alisema baada ya mafunzo yao ni vyema wakatambua na kujitambua wao wanaweza nini ili waweze kuwa juu.
“Haiwezi kuwa rahisi hata Yesu alibeba msalaba wake kukomboa watu wake” alisema akimaananisha kwamba ni vyema kuwa na maono ya unachotaka kama unataka kushiriki vyema.
Alisema kwamba wamejifunza elimu ya dijiti kama vile programu za Kompyuta (coding) na ujasiriamali wanachotakiwa kukifanya ni kufanya ubunifu wa miradi inayohusisha teknolojia na kuitumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yao kwa kuwa mitandao inaunganisha dunia.
Alisema kwamba kama mtoto wa kike akijielewa atatumia vyema fursa za uwekezaji zilizopo kwa kutumia vyema elimu anayoipta na kujiingiza katika ujasiriamali.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza kutia hamasa wasichana wa shule mbalimbali za sekondari nchini wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa Shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
 Mtaalamu wa Mawasiliano katika Sekta ya Nishati kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanazania, Johary Kachwamba akiwasilisha fursa za ubunifu katika sekta ya nishati wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Afisa Mipango wa Reach for Change Foundation, Bi. Jesca Mmari akizungumza na wanafunzi akiwataka kuwa na hamu na kujiamini katika kila kitu wanachotaka kukipata wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
 Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi.  Shamsa Suleiman akizungumzia kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Afisa Rasilimali watu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. John Mtega (kushoto) akizungumzia usawa wa kijinsia katika ajira na kuhamasisha wanawake kuomba nafasi za utumishi wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mhandisi wa Umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bi. Mkufu Shabaan (wa pili kushoto), Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi.  Shamsa Suleiman (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mipango wa Reach for Change Foundation, Bi.  Jesca Mmari (kulia).
Washindi wa kwanza wa shindano la ubunifu wa programu za kompyuta, ambao waliwasilisha wazo la changamoto za ukosefu wa taulo za  watoto kike mashuleni wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson (wa tatu kushoto),  Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Jaji Kiongozi wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (wa tatu kulia) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Washindi hao ni Eshe Mohamed (wa pili kushoto), Oliver Godliving (wa nne kushoto), Maleo Stanley (wa tano kulia) pamoja na Mwalimu Msimazi, Celestina Richard (wa nne kulia) kutoka shule ya Sekondari Kondo iliyopo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...