Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale anaeshughulikia masuala ya Habari Dkt. Saleh Yussuf Mnemo akizungumza katika khafla ya kuwaaga wafanyakazi hao iliofanyika ukumbi wa Palace Museum Forodhani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar Salum Kitwana Sururu akitoa shukurani zake kwa Wafanyakazi hao (hawapo pichani) na kuwatakia kheri katika maisha yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar anaeshughulikia masuala ya Habari Dkt. Saleh Yussuf Mnemo akimkabidhi cheti maalum Bi. Jokha Ali Simba mmoja ya wafanyakazi waliostahafu Idara ya Makumbusho ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZAPSU) Mwatumu Khamis Othman akimkabidhi saa ya ukutani mzee Mussa Vuai Pakia katika khafla ya kuwaaga wafanyakazi hao iliofanyika ukumbi wa Palace Museum Forodhani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale waliohudhuria katika ghafla ya kuwaaga wafanyakazi wenzao waliomaliza muda wa kufanya kazi katika Idara hiyo.
Wafanyakazi walioangwa baada ya kumaliza utimishi wao wa kazi katika Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar.
Picha na Abdalla Omar Habari - Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...