Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amesema hali ya upatikanaji majisafi na salama katika mji wa Longido wenye idadi ya wakazi 16, 712 inaongezeka kutoka asilimia 15 ya sasa inayowafikia wananchi 2, 510 hadi kufikia asilimia 100.

Waziri Mbarawa akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo amefafanua kuwa hatua hiyo inamaanisha wananchi wote katika mji huo watapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi mkubwa wa maji wa Longido unaoanzia mto Simba katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha Mita za ujazo 2,160 kwa siku wakati mahitaji halisi katika mji wa Longido ni Mita za ujazo 1,462.

Waziri Mbarawa ameainisha mradi wa maji Longido unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 15.7 tayari mabomba yenye urefu wa kilometa 94 yamelazwa kutoka katika chanzo cha maji cha mto Simba wilayani Siha na mkandarasi kampuni ya ujenzi ya STC anatakiwa kukabidhi mradi mwezi ujao Tarehe 15 Desemba 2018. 

Waziri Mbarawa amesema ili kuhakikisha wananchi wa Longido wanapata maji huduma ya maji haraka na kujikita katika shughuli nyingine za maendeleo, Serikali iliamua kandarasi ya mradi huo itekelezwe na Wakandarasi waliopewa kazi tofauti; kazi hizo ni pamoja na kujenga matanki, ujenzi wa mifumo ya kusambaza maji, na ujenzi katika chanzo cha maji.

Waziri Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama kama ambavyo Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini majisafi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. 

Aidha, ameongeza nia hasa ni kufanikisha asilimia 85 ya wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020 na asilimia 95 katika miji. Pamoja na hilo amewataka wananchi kutunza mazingira na kuotesha miti kulinda vyanzo vya maji. 
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akitoa maelekezo katika kizimba cha kupunguza msukumo wa maji (BPT) katika eneo la mto Simba, wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. Mradi wa maji wa Longido chanzo chake kipo mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiangalia ubora wa kizimba na bomba zilizotumika katika kizimba cha kupunguza msukumo wa maji (BTP) katika eneo la mashamba la Simba. BTP moja ya kazi yake ni kuzuia mabomba kupasuka. Mradi wa maji wa Longido mabomba yamelazwa kwa umbali wa kilomita 94 na thamani ya mradi ni kiasi cha Shilingi bilioni 15.7.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (Mb) akishiriki kazi ya kuunga mabomba kabla ya kulazwa eneo la Mbugani, katika mradi wa maji wa Longido . Waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi kampuni ya Ujenzi ya STC kukabidhi mradi ifikapo Tarehe 15 Desemba 2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...