Kilimanjaro.
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia amewamegea siri wananchi wa mji mdogo wa Himo juu ya mazungumzo yake na Rais Dk. John Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Alidai alikwenda kumueleza malalamiko ya wananchi kuhusu amri ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi ya kusitisha ujenzi wa barabara na kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi.
“Haya yote nimemueleza Mheshimiwa Rais (Magufuli) niwe mkweli, nilibahatika hapo katikati Mheshimiwa Rais akaniita akasema hivi, narejea sauti ya Rais aliniambia na ameshaagiza ofisi zake na wengine wameniita Dodoma, barabara za wana Vunjo atachangia yeye binafsi kama John Pombe Magufuli, pili serikali yake itachangia na tatu atakuja kama Amiri Jeshi Mkuu kufungua barabara hizi yeye mwenyewe kama John Pombe Magufuli,”alisema
Mbatia alikuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Makuyuni katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya ghalani.
Mradi wa upanuzi na ujenzi barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe unaodaiwa kusisitishwa katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zilikuwa zigharimu Sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) wa mwaka huu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...