Na Mwandishi wetu
MRADI mkubwa wa kufunza walimu wa wasimamizi wa mafunzo ya ufundi standi umezinduliwa kwa kufanyika kwa warsha itakayosaidia kutoa mwelekeo wa mradi .
Akizungumza katika warsha ya mradi huo wa BEAR ll unaofanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda katika awamu yake ya pili, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Noel Mbonde akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo alishukuru serikali ya Korea na UNESCO kwa kusaidia kupatikana kwa elimu hiyo nchini.
Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.
Alisema elimu hiyo itasaidia kuboresha na kuleta uwiano kati ya mafunzo ya ufundi stadi na matumizi yake katika viwanda nchini.
Alisema kuna malalamiko kwamba wahitimu wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika viwanda hivyo mradi huo ni msaada mkubwa.
Mradi huo wenye changio la dola za Marekani milioni 1.56 kwa kipindi cha miaka mitatu zinatarajiwa kusambazwa kwa mamlaka mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya ufundi stadi zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa mafundi stadi. Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Baraza la Ithibati (NACTE) nakadhalika.
Alisema mradi huo anaamini utatafuta tatizo la kutoa mafunzo kwa walimu wa ufundi na kuoanisha mahitaji ya viwanda.
Alisema ingawa awamu ya kwanza haikufika nchini Tanzania, awamu hii ya pili iliyoletwa nchini kwa miaka mitatu ina msaada mkubwa kwa watanzania ambao wanajiandaa kuwa nchi ya viwanda.
Pamoja na kushukuriwa, Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song amesema taifa lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba linawezesha elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo.
 Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumza kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Sehemu ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...