Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Kodi yatakayofanyika Novemba 17 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Isaya Jairo amesema katika mahafali hayo Naibu Waziri atakabidhi zawadi kwa wanafunzi 14 waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali.

Profesa Jairo amesema kuwa wahitimu kwa mwaka huu ni 359 na idadi imekuwa ikiongezeka kila kila mwaka kutokana na ubora wa elimu wanayoitoa.Amesema mikakati ya Chuo ni kuwa Chuo Kikuu kutokana na mahitaji ya Kodi na kuwa Chuo pekee kinachotoa utaalam wa kodi katika Afrika Mashariki.

Profesa Jairo amesema wahitimu 74 watatunukiwa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki pamoja na wahitimu 33 watatunukiwa cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 142 stashahada Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 wengine shahada ya uzamili katika Kodi na wahitimu 15 Postgraduate Diploma.

Katika mahafali hayo Naibu Waziri Kijaji atatoa vyeti kwa wahadhiri waliofanya tafiti na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya Kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Cha Kodi Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mahafali 11 ya Chuo hicho yatakayofanyika Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...