Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani leo tarehe 12 Novemba, 2018 amevunja rasmi Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Gideona Kaunda.

Uamuzi huo ameutoa katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma. Alisema kuwa, Bodi hiyo iliundwa mwaka 2017, kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini Na.8 ya Mwaka 2005 (The Rural Energy Act. No.8 of 2005). 

“ Bodi hii imetekeleza majukumu yake kwa takriban mwaka mmoja (1) sasa na katika kipindi hicho ambapo Bodi hii imekuwepo, ninapenda kuwajulisha kwamba kwa ujumla sijaridhishwa na utendaji wake,” alisema Dkt Kalemani.Hivyo alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 9(3)(b) cha Sheria Na. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005, ameamua kuivunja Bodi hiyo kwa kutengua uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi.

Aliongeza kuwa, Bodi nyingine mpya itaundwa baadaye kwa mujibu wa Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017 na ina wajumbe Saba.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuivunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...