Kwa nini usishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Pili linaloandaliwa na BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR) BAKIZA mjini Zanzibar  Desemba  12 na 13 mwaka huu? Upo usiku wa Riwaya ambapo utapata fursa ya kuonana  uso kwa uso, kupeyana mikono, kuongea naye hata kupiga picha na mwanariwaya maarufu Prof. Said Ahmed Muhammed aliyeanza kutunga riwaya "Asali Chungu" na "Nyuso za Mwanamke"

Hili Kongamano ni muhimu sana katika kuinua fasihi yetu. Kimsingi sasa hivi waandishi wa riwaya zenye mafunzo na maudhui ya kudumu na useful kwa vizazi vijavyo ni wachache sana...anaseme Dkt. Muhammed Seif Khatibu, Waziri Mstaafu na mmoja wa mabingwa wa lugha ya Kiswahili nchini.

"Kusipokuwa na namna ya kurudisha na kuonyesha kazi ya fasihi, itapotea moja kwa moja. Tutaendelea kuburudika na akina Amberuty kwenye instagram na akina Diamond na miziki yao..na fasihi yetu ndio itakuwa tumeichimbia kaburi moja kwa moja.."maneno ya msomi mmoja aliyeko China



 Njoo umwone, umsikilize, uongee naye, umshike mkono na upige picha naye mwandishi maarufu wa riwaya za Kiswahili ikiwemo Nyota ya Rehema na Kiu: Mohamed Suleiman Mohamed katika Kongamano la Pili la Kimataifa la  Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), mjini Zanzibar  Desemba  12 na 13 mwaka huu.
 Riwaya ya kwanza ya mwanariwaya Adam Shafi ilikuwa KULI lakini siku ya Kongamano atakizindua kitabu Kuona Mtoto  wa Mama. Fika umwone, umshike mkono,muongee na kupiga picha naye.Bahati ilioje! Ni  Desemba  12 na 13 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...