KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy (T) LTD kwa kushirikiana na Kampuni ya Air Tanzania Limited imezindua mradi unaojulikana kama “Sky is the Limit Project”wenye lengo la kuwatambulisha na kuwapa uelewa wanafunzi wa shule za msingi wasio na fursa au uwezo wa kuufikia kwa urahisi ulimwengu wa anga ili kuwapa uelewa kuhusu sekta hiyo yenye kuvutia.

Imeelezwa lengo la mradi huo ni kuwahamasisha watoto wanaotoka mazingira ya kawaida sana ya vijijini kwa kuwatia moyo katika masomo yao ili wajue na kuvutiwa na sekta ya anga na maeneo mengine ya fursa za kazi za nje ya maeneo wanaoishi.

Katika kufanikisha mradi huo zaidi ya wanafunzi 40 kutoka Shule za msingi za wilayani Kisarawe wamepata fursa ya kutembelea Shirika la Ndege la Air Tanzania pamoja na kushuhudia namna Kampuni ya mafuta ya Puma inavyohifadhi mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Mafuta ya Ndege Tanzania kutoka kampuni ya Mafuta ya Puma Illuminata Yateri amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa kama neon linavyojieleza la Sky is the Limit , mradi huo unataka kuamsha moyo wa ujasiri na kujiwekea malengo ya juu katika kufanikiwa.

Amefafanua mradi huo wa Sky is the limit utawapa wototo kutoka shule za msingi waliochaguliwa kutoka kwa jumuiya zisizo na fursa na uzoefu wa sekta ya anga kwa ukaribu zaidi, kwa kufanya ziara ya elimu inayofanywa katika miundombinu ya uwanja wa ndege kama ugavi wa mafuta ya ndege,huduma zinazotolewa kwenye ndege ,udhibiti wa safari za ndege, kupata habari mbalimbali za ndege kupitia watalaam wa sekta ya ana wanaohusika.

“Watoto watajua shughuli za kampuni ya mafuta ya Puma kuhusu biashara ya mafuta ya ndege jinsi yanavyouzwa kwenye ndege za ndani na za kimataifa.Kampuni ya Puma Tanzania ambayo ndio inayoongoza katika soko la kuuza mafuta ya ndege nchini imekuwa mshirika wa muda mrefu katika sekta ya anga katika kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
 ????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri (katikati) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Josephat Kagirwa (kulia) alipokuwa akizungumza na wanafunzi kutoka Shule za Msingi wilayani Kisarawe walipofanya ziara ya mafunzo uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni adhimisho la mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi kutoka wilaya yake wakati wa ziara ya kimafunzo kutembelea karakana ya ndege jijini Dar es Salaam jana kwa kushirikiana na Kampuni ya Puma Energy Tanzania katika kuhudumia utoaji wa mafuta ya ndege chini ya mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimfunga vifungo mmoja wa wanafunzi wakati walipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa JNIA katika mradi mradi ujulikanao kama Sky is The Timit
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Kisarawe, wakimsikiliza Injinia wa Ndege kutoka Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Nkhambi Salanga walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...