Windhoek, Namibia
Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".
Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru WAELE kwa tuzo hiyo na kwa kutambua mchango wake katika kusukuma agenda ya ushiriki wa wanawake katika uongozi. Amesema kuwa, hakufanya hivyo kwa kutegemea kupata tuzo siku moja, bali alitimiza wajibu wake wa uongozi wa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi kwa kuwa ni haki yao na sio fadhila. Amewashukuru wanawake aliowateua kaika uongozi kwa kutomuangusha katika madaraka aliyowapa.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mara baada ya kutunukiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitunikiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...