Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema haitasita kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote wanaopotosha jamii na vitendo vya uvunjifu wa maadili ya kitanzania kwa kujirekodi na kisha kusambaza picha za video za utupu mtandaoni.

Akizungumza leo Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA Joannes Karungura amesema kutokana na video inayosambaa kwa sasa nchini ikimuhisha msanii wa filamu nchini Wema Sepetu imeamua kumfikisha mahakamani ili asomewe shtaka linalomkabili na kwamba huo ni mwanzo tu kwani wote ambao wanaokiuka maadili mitandaoni watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Karungura amebainisha kuwa sheria zitaendelea kufuatwa na kwa yoyote atakayekiuka maadili ya kitanzania kama alivofanya Wema 
Sepetu na wengine ambao kesi zao ziko Kwenye taratibu kufikishwa 
mahakamani basi watatumikia kifungo cha miaka Saba au kutoa faini 
ya Sh.millioni saba.

Ametoa mwito kwa Watanzania kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha jamii yetu inakua na maadili,tabia njema pamoja na desturi nzuri ili kukijenga kikazi cha kesho na vinavokuwa maadili mazuri na hofu ya kutokufanya vitendo viovu.

Pia amewataka watu wenye picha pamoja na video chafu kufuta mara 
moja kwani TCRA wana mikakati mizito kwa watu ambao wanahifadhi 
pamoja na wanaosambaza picha hizo kuwafikisha Kwenye sheria 
ichukue mkondo wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...