Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi maalum wa kujaza nafasi ambazo zilizo wazi ndani ya klabunya Yanga ikiwemo ile ya Mwenyekiti.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea litaanza Novemba 8 hadi 13 2018 na wanachama wote watatakiwa kuhakiki majina yao kwenye matawi.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 2019. TFF wamemua kutangaza rasmi kuanza mchakato huo mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuwataka wausimamie wakieleza kuwa kamati ya Yanga haijitoshelezi.

BMT waliitaka TFF itimize majukumu hayo katika kikao na wanahabari kilichofanyika siku chache zilizopita.BMT iliiwataka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizuru huku ikiwemo ya Manji aliyeiandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Klau hiyo

Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe wanne kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.Viongozi waliojiuzulu ndani ya klabu hiyo ni Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na wajumbe Hashimu Abdallah, Salum Nkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi na huku waliobaki ni wajumbe Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika. 
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF , Ally Mchungahela akizungumza na waandishi kuhusiana na uchaguzi wa klabu ya Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...