Na Imma Msumba Arumeru,
MKUU wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerru Muro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo limewakamata watuhumiwa watatu ambao wameshiriki kumtoa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.
Akizungumza leo wilayani hapa, Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego ambao umefanikisha kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na mtia mimba ambao wamefikishwa polisi na kisha mahakamani
Akielezea jinsi alivyopewa ujauzito na mchakato wa kutaka kutolewa, mwanafunzi Aikaeli Pallangyo amesema ni kweli alipata ujauzito kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi nae jirani nyumbani ambae alikuwa akimrubuni kwa kumpatia fedha
Kwa upande wao watuhumiwa wa sakata hilo akiwamo kijana aliyempa mimba binti,pamoja na mama mzazi wa Aikaeli na mwanamke ambae ni ndugu wa Kijana aliempa mimba ambae anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito binti wametoa sababu mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe kwa zenyewe kutokana na mama wa binti kukiri kuwafahamu watuhumiwa wenzake na kuelezea tukio la mchezo mzima ulivyokuwa
Akidhibitisha taarifa za binti huyo kuwa mjamzito na kutoa ujauzito, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas kilasara amesema vipimo vya awali vilionyesha binti kuwa mjamzito na vipimo walivyofanya tena vimeonyesha binti sio mjamzito tena.
Ambapo amesema hata hivyo binti huyo ameendelea kupata dalili zote za kuwa na ujauzito ikiwemo ya maziwa kutoka. Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya usalama kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio hilo.Pia amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi 57 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...