Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga imekamata wahamiaji haramu 110 wakiwemo raia wa kigeni 103 na Watanzania saba kwa kuishi nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Novemba 14, 2018 Msemaji wa idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka 2018. 

Alisema wahamiaji hao haramu wengi ni kutoka katika nchi za jirani ambapo Burudi wamekamata 46, Rwanda wakiwa 13, pamoja na wengine kutoka nchi za Ethiopia, Kenya,India na China.

"Katika kipindi cha miezi mitatu,tumekamata na kuhoji watu 110 kati yao raia wa kigeni wakiwa 103 na Watanzania saba,kati ya wageni hao 103, wahamiaji 43 wamerudishwa kwenye nchi zao na 60 walibainika kuwa na vibali halali hivyo kuwaruhusu kuendelea kuishi hapa nchini",alieleza Mwanawina. Aliyataja maeneo ambayo wamekamata wa hamiaji haramu wengi kuwa ni wilaya ya Kahama kwenye mashamba ya Tumbaku, Mpunga na migodi na kwenye mgodi wa Mwakitolyo uliopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Naye Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena, aliwataka watanzania kuachana na tabia ya kuhifadhi wahamiaji haramu, ambao wamekuwa wakivuruga amani ya nchi. Katika hatua nyingine aliwahimiza watanzania kila mmoja ajitahidi kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA), ambapo itafikia kipindi bila ya kuwa na kitambulisho hicho watakosa huduma za kijamii ikiwemo matibabu, lengo likiwa ni kukomesha kuwepo kwa hawamiaji haramu hapa nchini. 
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga leo ofisini kwake.
Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena akielezea kuhusu Operation wanazoendelea nazo kushughulika na wahamiaji haramu.Picha na Marco Maduhu Malunde1 Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...