Na Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanza kwa Operesheni kali ya kuwabaini na kuwasaka watu wote wanaojihusisha na wizi wa mafuta katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi wa reli hiyo katika kambi ya ujenzi ya Soga mkoani Pwani na Ngerengere wakati wa ziara yake katika mradi huo kufuatia kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mafuta.

Sabas amesema Operesheni hiyo haitamwacha salama yeyote atakayekutwa akishiriki na kufanikisha vitendo vya wizi katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao kuwa wa kwanza kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya wizi katika maeneo yao ili mradi huo uwe salama.

“Polisi tutatumia kila aina ya nguvu zetu kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa salama na tukikamata mwizi wa mafuta katika mradi huu hatasahau maisha yake yote kwa kuwa kuhujumu mradi huu muhimu kwa taifa ni kosa kubwa hasa ukizingatia gharama kubwa ambazo Serikali inatua kufanikisha jambo hili” Alisema Sabas.
Katika hatua nyingine DCP Sabas amewaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Pwani na Morogoro kuweka mikakati kabambe kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Reli ili kufanya doria za mara kwa mara katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kwa kuwa ndipo kulikobainika kuuzwa mafuta ya wizi wa mradi huo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli amesema wamekuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara na wadereva wa mitambo na magari katika mradi huo kwa lengo la kuwataka kushiriki katika kutoa taarifa za wizi na kuacha kujihusisha na vitendo hivyo ambapo waliokamatwa tayari wamefikishwa Mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...