Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali
ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.

Ndege
mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa
maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya
kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa
Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini
mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300
itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege
mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla
iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Desemba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi
wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300
ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job
Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi
Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa
Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla
iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Desemba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi
Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La
ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya
Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika
Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...