Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu cha Rais Dkt.John Magufuli kumekuwa maendeleo ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa miundombinu mbalimbali.
Akizungumza na waandishi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho Raymond Mwangwala amesema tunakwenda katika uchumi wa kujitegemea zaidi.
Amesema kwa sasa ndege tano ambapo ni faida kwa watanzania kupata maendeleo kwa kuingia katika biashara ya usafiri wa anga.Mwangwala amesema sasa ni mapigano ya uchumi hivyo Umoja utamlinda katika kwenda na uchumi huo kwa kasi.
Amesema ndege iliokuja ni ya kwanza kwa nchi za Afrika hivyo kila mtanzania anatakiwa kupongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli.Ametaja miradi mikubwa ambayo inafanywa na serikali ya awamu ya tano ikiwa mradi mmoja umeshakamilika na miradi mingine ni Ubungo, Salender na Mradi wa Reli ya Kisasa SGR.
Amesema kuwa Demokrsia iliyopo lazima kuwa na mipaka hivyo kila mtu lazima kufuata sheria katika kuitumia Demokrsia hiyo pamoja na kumsaidia Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha amesema baadhi ya vijana wanatumika na mataifa ya nje na kusahau uzalendo wa nchi."Vijana wa CCM tutakuwa wa kwanza kumlinda Rais Wetu ili kuweza kufikia uchumi wa kati"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Raymond Mwangwala akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kupongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika maendeleo mbalimbali yaliyotokea katika kipindi cha miaka mitatu, leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...