Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mufti wa Tanzania kwa namna ambavyo uongozi wake umemaliza migogoro ambayo ilikuwa inaibuka kwenye misikiti mbalimbali nchini na kwamba kwa sasa Waislamu ni wamoja.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hali ya amani nchini ambayo msingi wake unatokana na viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakihimiza umoja na mshikamano.

Majaliwa amesema hayo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za BAKWATA kufikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968 ambapo amesema dini zote zimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika maendeleo nchini.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Mufti wa Tanzania ambavyo chini ya uongozi wake ambavyo amesaidia kuwafanya Waislamu nchini kuwa wamoja na kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yao.

"Leo hii tunashudia chini ya Mufti wa Tanzania,hatusikii migogoro ambayo tulikuwa tunaisikia siku za nyuma.Kumetulia na mambo yanakwenda vizuri.Hongera Mufti Sheikh Aboubakary Zubeiry kwa uongozi wako mahiri.Tangu uwe kwenye nafasi hiyo sasa ni mwaka wa tatu,umetuunganisha ," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Wakati huo huo amezungumzi mchango wa viongozi wa dini zote pamoja na waumini wa dini hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...