Na, Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Ametanabaisha kuwa akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu kuliko mgodi wote, ‘kuliko mtanzania mmoja afe ni bora huo mgodi usiwepo’.

Aliyasema hayo leo tarehe 04 mwezi Januari alipokuwa akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara inayoendelea kwa siku mbili.

Biteko alibainisha kuwa, Buhemba ni eneo linaloongoza kwa ajali kwenye migodi, huu mgodi ulifungwa na toka umefunguliwa kuna vifo vya wachimbaji kumi na mbili na majeruhi 20, Serikali haiwezi ikakubali hali hiyo iendelee “Mimi nakwambia mwenyekiti sitakubali hali hii iendelee mimi mwenyewe nitakuja kuufunga tena mgodi huu kama hali hiyo itaendelea hatuwezi kupoteza maisha ya watanzania” Biteko alisisitiza.

Biteko aliongeza kwa kusema, Serikali haiko tayari kuona kuwa watu wanaendelea kufa ndio maana imeamua kufika na kuandaa mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili waweze kufundishwa namna bora za uchimbaji salama na wenye tija. Biteko alisema mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya, na mazingira ya uchimbaji katika mkoa huu wa Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) alipofika ofisini kwake kuelezea uwepo wake katika wilaya hiyo.  
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza jambo mbele ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kuboresha uchimbaji wao yanayofanyika katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara. 
Baadhi ya Wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao yenye lengo la kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa Madini yanayoendelea katika wilaya ya Butiama mjini Buhemba mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushota) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kujikita katika uchimbaji wenye tija.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...