Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefadhaishwa kwa kukosekana kwa afisa wa TRA katika Kituo cha Kibiashara cha Pamoja ambacho lengo lake ni kurahisisha shughuli za kibiashara kwa wananchi wa Wilaya ya Kigoma kwa kupata huduma zote za uwezeshaji wa biashara katika eneo moja.

Licha ya kuwepo kwa kituo hicho kilichojengwa na kukamilika tangu miezi sita iliyopita lakini afisa kutoka TRA anakosekana licha ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ujiji kufanya mawasiliano na TRA kwa miezi sita hadi sasa.

Kituo hicho ni miongoni mwa miradi kadhaa iliyo chini ya mradi wa Local Investment Climate(LIC) unao ratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kutokana na hali hiyo waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kigoma kufanya ufuatiliaji wa haraka ndani ya siku nne ili kituo hicho kiweze kuwa na Wadau wote wa kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma ya kuanzisha na kuratibu biashara zao kwa haraka. 


Imesemekana kwamba TRA walishafika kituoni hapo na kuahidi kuleta Afisa mmoja lakini hadi leo bado jambo hilo halijafanyika hivyo kuleta usumbufu kwa wafanya biashara wanaohitaji huduma kutoka katika kituo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kigoma ndani ya kituo cha Biashara kilichopo Wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akikagua kituo cha uwezeshaji wa biashara kilichopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akipokea taarifa ya uendeshaji wa kituo cha biashara toka kwa watendaji wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...