Na Felix Mwagara, MOHA-Karagwe.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Karagwe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Changarawe mjini humo, Lugola alisema kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu katika mikoa hiyo, hivyo CGI na Maafisa wake wahakikishe wanawaondoa wahamiaji wote haramu kupitia operesheni kubwa niliyoitangaza. “Nimepata taarifa na ndani zaidi na pia nyie wananchi hapa mmesema leo kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, ndio mana nimekuja hapa kwa ajili ya kuhakikisha wahamiaji hao wanaondolewa haraka iwezekanavyo hapa Kagera na Mkoa wa Kigoma,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, licha ya kutangaza operesheni hiyo, lakini viongozi wa uhamiaji katika mikoa hiyo wawe makini mara kwa mara kuhakikisha wanawafuatilia wahamiaji hao kwa kuwashirikisha wananchi waaminifu ili waweze kutoa taarfia sahihi za wahamiaji hao. “Tunatarajia kufanya uchaguzi hivi karibuni mwaka huu, hivyo mnapaswa kuhakikisha watakaopiga kura ni Watanzania na sio wenginevyo ili kuepusha usumbufu mkubwa katika jamii,” alisema Lugola.
Serikali hii ya Magufuli haichezewi na haijaribiwi, ole wako wewe afisa uhamiaji uingie mikononi mwangu, sitakuonea huruma na hakika nitakuondoa kazini,” alisema Lugola. Lugola alisema wahamiaji haramu sio wakuchekewa hivyo amemtaka CGI ahakikishe anawapanga vizuri nmaafisa wake kwa kutembnea nyumba kwa nyumba kuwasaka na kuhakikisha wote wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa mjini Karagwe Mkoani Kagera, katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa Changarawe mjini humo, leo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi hao, amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Mji wa Karagwe, Mkoani Kagera, Clemence Ishelenguzi alipokuwa anatoa kero zake mbalimbali katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Changarawe mjini humo, leo. Lugola katika hotuba yake, amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...