Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa timu ya Yanga Heritier Makambo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019 ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Makambo , alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Miraji Athumani wa Lipuli ya Iringa na Idd Selemani wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL.
Kwa mwezi huo wa Desemba, Yanga ilicheza michezo mitano, ambapo Makambo alitoa mchango mkubwa kwa Yanga kupata pointi 15 ikishinda michezo yote mitano iliyocheza, huku mshambuliaji huyo akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne.
Kwa upande wa Miraji Athumani alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu ya Lipuli kwa mwezi huo, ambapo timu yake ilicheza michezo minne ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja ikijikusanyia pointi 10 na kupanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya nane, huku Idd Selemani naye alionesha uwezo wa hali ya juu kwa timu yake ya Mbeya City kwa mwezi huo.
Pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Lipuli, Samuel Moja na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime aliongia nao fainali. Zahera aliiongoza timu yake katika michezo minne kati ya mitano iliyocheza, ambayo Yanga ilishinda michezo yote mitano na kuvuna pointi 15 hivyo kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikipanda kutoka nafasi ya pili.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa timu ya Yanga Heritier Makambo ambaye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019 ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...