Na Emanuel Madafa, Mbeya 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoa wa Mbeya, imemfikisha Mahakamani mtumishi wa Wakala wa Barabarani(TANROADS) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi 597,000.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Kiyano, alisema mtumishi huyo akiwa msimamizi wa mzani wa kupima magari uliopo eneo la Uyole Jijini Mbeya, alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mtumishi wa Kampuni ya Kichina iitwayo Chongqing Foreign Trade Economic Corporation.

Amesema Kesi hiyo namba CC. 189/ 2018 imefunguliwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya, chini ya kifungu cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 dhidi ya mtumishi huyo wa umma Zabron Zebeda Kenan.

Ameeleza kuwa mtumishi huyo wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani, inasemekana alitoa kiasi hicho cha fedha ili gari aina ya Howo lenye namba za usajili T 755BZC na Tela namba T587BPY lililokuwa halina kibali cha mzigo wenye upana usio wa kawaida(Abnomal Wide Loard) lipite kwenye mzani huo bila ya kukamatwa.

Aidha,Mkuu huyo amesema , Taasisi hiyo inaendelea kumtafuta mtumishi wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani kwani alifanikiwa kutoroka baada ya kutoa hongo hiyo, huku gari yake aina ya Toyota Carina lenye namba  T108 BQH likishikiliwa na ofisi hiyo ya TAKUKURU.

"Baada ya kutoa fedha hiyo Ngonyani alitoweka na kukimbilia Mahali pasipo julikana ambapo tulifanikiwa kumamata gari anayo tumia hivyo tunamtaka afike na achukue gari lake "Alisema Kiyabo.

Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa gari hiyo, iliponunuliwa haikubadilishwa umiliki wake hivyo kuna fedha ya serikali inatakiwa kulipwa kama ada ya kuhamisha umiliki na endapo ataendelea kujificha chombo hicho cha moto kitapigwa mnada ili kufidia gharama za serikali.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Takukuru Mbeya amesema katika roho ya Tatu ya mwaka 2018/2019 taasisi hiyo imeendelea kuchambua mifumo katika utendaji wa serikali ,mashirika ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuzuia mianya ya rushwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...