Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi. 

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa kikao mkakati baina yake ya mamlaka za ukusanyaji wa kodi ambapo amesema mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuwa kinara.Aidha RC Makonda amewataka watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza idadi ya walipa kodi, kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi Kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshauri kuanzisha kwa kitengo cha ushauri kwa wafanyabiashara jambo litakalowajengea wananchi hamasa ya kulipa kodi na kuondoa dhana ya kuonekana ni watu wa kukusanya mapato pekee.

RC Makonda anaamini kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi serikalini endepo watawekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kulipia ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuwekwa katika data base moja.

Kikao hicho kimehusisha wakuu wa wilaya, makatibu tawala, TRA, BOT, TIC, NBS, Wizara ya fedha na kamati za ulinzi na usalama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na na Watendaji kuhusu kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...