Na Imma Msumba Arumeru

Wananchi wa Kata ya Oldonyowasi Wilayani Arumeru wameitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuchangia miradi ya maendeleo kwa kuchanga zaidi ya sh. milioni 22.8 ili kuondoa adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kusaka elimu. 

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Cornel Muro pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dkt. Wilson Mahera katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana wilayani Arumeru.

Pongezi za Wananchi hao zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye yupo katika ziara Wilayani Arumeru baada ya kujionea changamoto za upungufu wa madarasa sambamba na kuzitatua ili Januari saba mwaka 2019 wanafunzi hao waweze kuingia madarasani kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza. 

Rc Gambo alisema juhudi walizozifanya wananchi hao wa Kata ya Oldonyowasi zinapaswa kuigwa na wananchi wengine kwani wamejitolea nguvu kazi watu pamoja ni fedha za wadau wa maendeleo ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) waliotoa sh. milioni 237 pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) waliotoa sh. milioni 30, akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Aminah Mollel kutoa mifuko kadhaa ya saruji huku Halmashauri ya Arusha Dc ikitoa sh. milioni 20.

Alisema tayari ameshaandika barua Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwaajili ya kuomba usajili kwa shule kadhaa za Mkoa wa Arusha ikiwemo shule hiyo ya Oldonyowasi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma badala ya kukaa nyumbani wakisubiri usajili wa shule huku wakikosa vipindi madarasani. "Nawapongeza kwa ushirikiano kati ya DC Muro na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dkt. Wilson Mahera pamoja na wananchi ambao mnajitajidi kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa kujenga madarasa naomba ushirikiano huu udumu zaidi ili wananchi mfaidi matunda ya elimu bure "

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Ndugu Jerry Cornel Muro amempongeza Rc Gambo kwa kuhakikisha shule hiyo inapata usaili na kusisitiza kuwa shule hiyo itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita ili watoto wa Kata hiyo na kata nyingine za Jirani waweze kupata elimu. Awali Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari, Nelson Saro alisema halmashauri ya Arusha Dc wanafunzi 6,846 walifaulu wakiwemo wasichana 3,884 na wavulana 2,962.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro wakiwa wameambatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wakikagua madarasa Wilayani Arumeru.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro wakiwa katika moja ya shule walizozitembelea kukagua ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Arusha Dc Wilayani Arumeru

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...