Na Mwandishi Wetu, MOHA-Karagwe.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili.
Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili kupandishwa vyeo na kurekibishiwa mishahara hivyo askari hao wana haki kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, mjini Missenyi na Karagwe Mkoani Kagera, leo. Lugola alisema alitoa agizo kuwa ifikapo  mwezi Agosti mwaka jana agizo hilo liwe limefanyiwa kazi, lakini mpaka umefika mwaka mpya bado halijafanyiwa kazi.
“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini.” Alisema Lugola. Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. Magufuli anatoa mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa nyumba hizo.
“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,” alisema Lugola. Pia lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Wallace Mashanda, wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Wilaya hiyo, leo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Luteni Kanali Denice Mwila. Lugola katika kikao chake na Baraza la Askari wilayani humo, aliwataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Luteni Kanali Denice Mwila akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya huyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, jana. Katika hotuba yake Waziri Lugola aliwataka Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera. Lugola aliwataka wananchi wa mji huo wahakikishe wanafuata sheria za nchi kwa kuwa nchi ipo salama. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Wilayani humo, Balozi Dkt. Deodarus Kamala, ambaye alipandishwa jukwaani na Waziri huyo ili aweze kuzungumza na wananchi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...