Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma zake za DStv imetangaza tena ofa mpya na kabambe kwa wateja wake inayojulikana kwa jina la  “Step Up”  ambapo mteja wa DStv atatakiwa kufanya malipo ya mwezi ya kifurushi cha juu ya kile anachotumia  na kisha kupatiwa  kifurushi cha juu zaidi ya kile alicholipia kwa kipindi cha mwezi mzima bila malipo ya nyongeza.

Akizungumza wakati wa kutangaza ofa hiyo Meneja Uendeshaji wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo alieleza kuwa Ofa ya‘Step Up’ ni kampeni maalum kwa wateja wa DStv yenye lengo la kuwatunuku wateja wanaolipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia.  Wateja wa vifurushi vya Bomba, Family na Compact watakaolipia kifurushi kinachofuatia juu yake watatunukiwa kufurushi cha juu zaidi. Kwa mfano, mteja wa Bomba akilipia kifurushi cha Family atazawadiwa kifurushi cha Compact. Mteja wa Family akilipia Compact anapata kifurushi cha Compact+ na yule wa Compact akilipia Compact+ anapewa kifurushi cha Premium”, alisema Shelukindo.

Aliongeza kuwa” Kampeni hii ya “Step Up” itadumu kwa kipindi cha muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 March 2019 hadi tarehe 30 Aprili 2019 na itawahusisha  wateja wa Wateja wote ambao akaunti zao hazijakatika vifurushi vya Bomba, Family pamoja na kile cha Compact.
 Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akitangaza rasmi promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili itaishia mwisho wa mwezi wanne.
  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akielezea  promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa muda wa miezi miwili.  Kulia ni Meneja Uhusiano Johnson Mshana na katikati ni Meneja Uendeshaji Ronald Shelukindo.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akieleza kuhusu promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa muda wa miezi miwili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...