SHIRIKISHO la Riadhaa Duniani (IAAF) limekana kwamba litaiambia Mahakama kuwa
wanariadha wote wanawake wenye viwango vikubwa vya homoni za kiume mwilini,
yaani testosterone kama vile Caster Semenya wanapaswa kutambuliwa kama
wanaume.
Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 anapinga sheria
iliyopendekezwa na IAAF inayonuiwa kudhibiti viwango vya homoni hiyo kwa
wanariadha wanawake. Kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya malalamiko katika
michezo (Cas) wiki ijayo.
Gazeti la the Times limeripoti kuwa mawakili wa IAAF watasema kuwa Semenya
"kibayolojia ni mwanamume" pamoja na kwamba anatambuliwa kuwa mwanamke.
Shirikisho hilo la riadha linasema "halitambui" mwanariadha yoyote mwenye "tofuati
za kukuwa kijinsia" (DSD) ambapo raia wa Afrika kusini, Semenya ndiye
anayeonekana zaidi kuwa mwanamume .
"Kinyume na hicho, tunakubali jinsia zao kisheria pasi na shaka, na tunawaruhusu
washiriki katika kitengo cha wanawake," lilisema siku ya Jumatano.
"Hata hivyo, iwapo mwanariadha aliye na hali hiyo ya DSD, atakuwa na sehemu nyeti
za kiume, na viwango vya kiume vya homoni hiyo ya testosterone, wanapata
ongezeko la mifupa na uzito wa misuli na nguvu na huongeza damu mwilini ambayo
mwanamume hupata wanapo baleghe, ndicho kinachowapatia wanaume nguvu zaidi
ya wanawake katika mashindano.
"Kwahivyo, ili kuwa na ushindani wa sawa katika kitengo cha wanawake, ni muhimu
kuwataka wanariadha walio na hali ya DSD kuzipunguza homoni kusalia kuwa kama
za wanawake kabla hawajaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa"
IAAF ilinuia kuuidhinihsa sheria mpya Novemba 1, 2018 lakini ikaahirisha hadi
Machi 26 kusubiri matokeo ya kesi aliowasilisha Semenya na Shirikisho la Riadha
Afrika Kusini.
Kuahirishwa huko kunamaanisha kuwa wanariadha wenye hali hiyo ya DSD
hawatoruhusiwa kushiriki katika mashindano kwa miezi 6 kutoka tarehe ambayo
mabadiliko ya sheria yataidhinishwa ambayo, huenda ikamfanya Semenya akakosa
kushiriki baadhi ya mashindano ya msimu wa nje 2019.
Hata hivyo wakati Semenya, alipotangaza kwamba atapambana na sheria hizo
mwaka jana Afrika kusini alisema: "Si haki. Nataka nikimbie kama kawaida, namna
nilivyozaliwa. Mimi ni Mokgadi Caster Semenya. Mimi ni mwanamke na nina kasi."
Wakati huohuo Mtafiti Mkuu Mwenza katika Chuo Kikuu cha Yale na Mtaalamu Mkuu
wa masuala ya homoni hiyo ya testosterone
Katrina Karkazis ni miongoni mwa walioshutumu shirikisho hilo la riadha duniani
kuhusu msimamo wake.
Amesema IAAF "inatafasiri vibaya sayansi ya bayolojia ya jinsia" na inatafuta "kuunda
ufafanuzi wake binafsi wa jinsia kutokana na imani zenye makosa kuhusu bayolojia
na jinsia," na kuongeza hilo halina msingi na linaweza kuwa na madhara zaidi kwa
kuidhinihsa ukosefu wa uelewa na kuchangia unyanyasaji zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...