Je, unafahamu kwamba unaweza kujiajiri kupitia Jumia?
  • Pata kamisheni kwa kuuza bidhaa zinazopatikana Jumia.
  • Zaidi ya mawakala 600 wamekwishajiunga.

Timiza ndoto zako za kibiashara kwa kujipatia kipato zaidi na zaidi! Kuwa bosi wako mwenyewe kwa kufanya shughuli zako na kujiingizia kipato bila ya mtu kukusimamia. Ndiyo kauli mbiu ambayo Jumia inaitumia kwa sasa katika kuwahamasisha vijana wa kitanzania kutumia fursa zilizoletwa na teknolojia kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

Kampuni hii ambayo inajishughulisha na kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni Tanzania imeanzisha programu inayokwenda kwa jina la ‘Jumia JForce.’ Huu ni mtandao wa wataalamu wa ushauri wa mauzo ambao hujiingizia kipato kwa kuwasaidia wateja kufanya manunuzi ya bidhaa zinazopatikana kwenye tovuti ya Jumia. Kwa sasa kuna mawakala takribani 600 waliotapakaa Tanzania nzima.
Changamoto ya ajira ni kubwa duniani kote na sio nchini Tanzania pekee au barani Afrika kwa ujumla. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Afrika ya mwaka 2019 iliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, imeainisha kuwa nguvu kazi ya Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa 40% zaidi kufikia 2030. Inaendelea zaidi kwa kufafanua kuwa, endapo mienendo iliyopo sasa ikiendelea, ni nusu pekee ya nguvu kazi mpya inayoingia ndiyo itakayopata ajira, na ajira nyingi zitakuwa kwenye sekta zisizo rasmi. Hii ina maanisha kwamba vijana takribani milioni 100 watakuwa bila ya ajira.

Akifafanua namna Programu ya Jumia JForce inavyoweza kuwa mwarobaini wa changamoto ya ajira kwa vijana, Nahodha wa Wakala wa Mauzo wa Jumia - Tanzania, Bi. Elizabeth Samson amesema kuwa, “Kuwa bosi wako mwenyewe, ‘kamwe usiseme haiwezekani.’

Mwaka mmoja nyuma kama angekuja mtu na kuniambia kuwa unaweza kujiingizia kipato cha zaidi ya laki moja na kuendelea kwa kujifanyia shughuli zako mwenyewe, ningemwambia apeleke hizo hadithi kwa ndege wa mwituni. Mtu pekee ambaye anaweza kukuzuia kufanya hivyo ni wewe mwenyewe. Kwa mafunzo na nyenzo zinazopatikana Jumia JForce, ni rahisi kuanza kuingiza kipato mara moja na kukuza mapato yako kwa urahisi, hakuna kuwekeza mtaji kabisa. Kama wakala wa JForce, unaweza kuwa vile unavyotaka kuwa, ishi ndoto zako na ujenge mustakabali wa baadaye!”

Programu ya mawakala wa mauzo kutoka Jumia ina malengo ya kuwapatia uwezo na kuwaimarisha watu wanaotarajia kuwa wajasiriamali kwa kuwapatia msaada wa kukuza biashara zao. Jiunge kwa kulipia gharama ndogo na kisha uanze kuingiza kipato kwa kuuza bidhaa za Jumia zinazokuzunguka.

Faida 5 za kujiajiri kupitia Jumia JForce

Unajiingizia kipato chako mwenyewe. Unapata kamisheni kwa kuuza bidhaa zinapatikana katika tovuti ya Jumia kutoka kwa wauzaji tofauti. Unalipwa kutokana na juhudi zako za kuweza kuwashawishi wateja wengi zaidi kununua bidhaa: kadri unavyofanya kazi, ndivyo unavyolipwa zaidi!

Bosi ni wewe mwenyewe. Ukiwa kama wakala wa programu ya mauzo, una uhuru kamili na udhibiti wa shughuli uzifanyazo. Jenga biashara yako yenye kukunufaisha wewe mwenyewe. Hakuna cha kukuzuia! Pia, unaunda timu yako mwenyewe ya mawakala wa mauzo ambayo itakuwa inaripoti kwako na kuisimamia.

Unapatiwa mafunzo bure. Kadri unavyokua ndivyo unavyozidi kujiongezea malipo ya kamisheni. Utapatiwa ujuzi na mafunzo ya hali ya juu. Utanahakikishiwa kwamba unakuaa mfanyabiashara uliyewezeshwa kikamilifu.

Unafurahia kile unachokifanya. Uza bidhaa na uzawadiwe. Pata maarifa mapya na ujijengee uwezo wa kujiamini. Kutana na watu wapya na utengeneze marafiki wapya. Pata fursa ya kuhudhuria matukio ya Jumia kama vile hafla, semina na warsha mbalimbali.

Faida. Pata fursa ya kujua promosheni za kila siku. Furahia kujipatia kipato kupitia kulipwa kamisheni. Shiriki bure mafunzo yote ya Jumia na ujipatie ujuzi wa kazi yako! Hauhitajiki kuwa na uzoefu, bali msukumo na shauku kubwa ya biashara!

Unasubiri nini kuichangamkia fursa hii? Ikiwa ndio mwanzo wa mwaka wa 2019 ambao umejaa fursa lukuki siku za usoni ni vema kufanya maamuzi ya kujiunga sasa. Kwasababu hivi punde kampeni mbalimbali za mauzo zinatarajiwa kuzinduliwa ikiwemo ya msimu wa wapendao au ‘Valentine’s’ ambayo inatarajiwa kuanza Februari 4 mpaka 16.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...