Kituo cha afya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa dawa ambazo hupelekwa kidogo ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho huku tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi vikiendelea kutokea katika kituo hicho.
Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Yahya Mohamed ametoa taarifa hiyo baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo dawa za kusaidia kina mama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua na vifaa vya upasuaji kwa kina mama wanaopata uzazi pingamizi kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam.
Amesema kituo hicho kwa sasa kinahudumia idadi kubwa ya wagonjwa hasa wasiokuwa na uwezo hivyo wakati mwingine kulazimika kutoa huduma ya matibabu bure kwani hawawezi kumwacha mgonjwa apoteze maisha kwa sababu tu hana fedha za kulipia
Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo kutoka OGG Liku Madaki ameelezea kuwa  lengo la msaada huo ni kuutaka uongozi wa kituo hicho kuitumia kwa lengo lililokusudiwa ili kuokoa maisha ya wana Ikwiriri na Rufiji kwa ujumla,mbali na vifaa na dawa amesema wamepeleka zawadi mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa:
Baadhi ya wagonjwa  kituoni hapo mbali na wakishukuru kwa msaada huo,ambapo pia wameiomba serikali kuboresha kituo hicho kwa kuhakikisha kinapata vifaa na dawa kulingana na idadi ya wagonjwa ili kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma ya matibabu Utete ambako kuna hospitali ya wilaya.
Mdau wa Afya Ufoo Salo kutoka kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam akikabidhi baiskeli ya wagonjwa kwa Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Yahya Mohamed.
Mdau wa Afya Ufoo Salo kutoka kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam akiwa amemshika mtoto walipotembelea kituo cha afya Ikwiriri, Rufiji Mkoani Pwani .

 Baadhi ya Wadau wa Maendeleo kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam,wakijadiliana jambo kala ya kuanza shughuli yao ya kukabidhi msaada waoo vifaa tiba na vitu vingine kwa kituo hicho cha Afya. 
 Baadhi ya Wadau wa Maendeleo kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam,wakikabidhi msaada waoo vifaa tiba na vitu vingine kwa Uongozi wa kituo hicho cha Afya. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...