Na Ripota Wetu, Dar es Salaam.
Mkazi
wa Keko jijini Dar es Salaam, Yusuph Julla, ameibuka na ushindi wa sh
milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya biko, huku akimchagua mke wake
Mwanaidi Salumu kuwa mpendanao wake kutokea kwenye vuna fedha za
wapendao.
Makabidhiano
hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam, kwa kuwakabidhi chao wapendanao
hao wenye maskani yao Keko wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ili
waendelee na harakati zao za kimaisha.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Julla aliishukuru Biko kwa kumpatia fedha
zake mapema akisema kuwa fedha hizo zitawanufaisha yeye na mkewe kwenye
familia yao hiyo.
Kucheza
Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake
ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500
wakati watakaocheza kwa sh 1000
na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo
kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye
droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.
Bahati
nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo
Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050
na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi
kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.
Mshindi
wa sh milioni 10 kutoka Bahati nasibu ya Biko, Yusuph Julla, akiwa na
mkewe baada ya kukabidhiwa fedha zake za ushindi kutoka kwenye bahati
nasibu hiyo huku Julla akimtaja mkewe Mwanaidi Salimu kuwa mpendanao
wake hivyo kugawana fedha hizo kwa pamoja kwa ajili ya kufanyia mambo ya
kimaendeleo. Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi huku
washindi wa droo kubwa wakipatikana Jumatano na Jumapili pamoja na
zawadi za papo kwa hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...