Na WAMJW-DAR
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetangaza nia ya kuanza kujenga vituo vya utengamao kwa watoto wenye
ulemavu nchini (Rehabilitation Centers).
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha
utengamano wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku( Community Based
Rehabilitation Centre) kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
“Ninaahidi
kwenye kila kituo cha afya cha serikali ni lazima tuanze kujenga
majengo ya utengamao kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, tuna takribani
vituo vya afya 510 nchini tunaweza tusijenge kwenye vituo vyote kwa
wakati mmoja lakini naamini tunaweza tukaanza na vituo vya afya 50”.
Amesema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy amesema kuna changamoto za kupata takwimu sahihi za watu wenye
ulemavu ambapo kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha
watu wenye ulemavu nchini ni asilimia 5.8 na kati ya hao asilimia 60 ni
watoto chini ya miaka 18.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Ummy ameomba wadau mbalimbali wa Afya waweze
kusaidiana na Serikali katika kutekeleza azma ya kujenga vituo hivyo,
lengo likiwa ni kuwafikia wanawake na walezi wengi wenye watoto wenye
ulemavu nchini.
Waziri
Ummy amesema kuna uhaba mkubwa wa vituo vya Utengamao nchini huku
akitoa mfano wa Jiji la Dar Es Salaam lenye vituo visivyozidi 6 lakini
idadi ya watu ikiwa ni zaidi ya Milioni 5. Hata hivyo Waziri Ummy
ameupongeza uongozi wa Kituo hicho cha Kila Siku Community Based
Rehabilitation kwa kuanzisha huduma za utengamao kwa watoto wenye
ulemavu na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wenye ulemavu
kwenye vituo hivyo kuliko kuwafungia ndani.
Aidha,
Waziri Ummy ameagiza Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoa elimu
kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kwenye maeneo yao ili
kuondoa dhana potofu ya kufungia ndani watoto na kuwanyima haki zao za
msingi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo kutoka
nchini Italia Bw. Michelangelo Chiurchiu amesema lengo la kuanzishwa
kituo hicho ni ujumuishwaji kwa wote wenye lengo la kuboresha maisha ya
watu wenye ulemavu kupitia uboreshaji wa huduma za utengamao kijamii,
kujenga uwezo wa kiuchumi kwa watu wenye ulemavu pamoja na ujumuishwaji
wa watoto wenye ulemavu katika elimu ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akifungua jiwe la msingi lililowekwa katika ujenzi wa kituo kipya cha
utengamao wa watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
Kushoto ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni na
katikati ni Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw.
Michelangelo Chiurchiu


Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akisalimiwa na mmoja wa watoto wenye ulemavu wakati alipotembelea maeneo
wanapofundishwa utengamao katika kituo cha utengamao cha Kila Siku
kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi
ya wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu wakifuatilia hotuba
mbalimbali zilizotolewa katika ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa
watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto
wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar. Kushoto ni Mkuu
wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu na
Kulia ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akisikiliza jambo alilokua akielezwa na Mkuu wa Shirika la Comunita
Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu wakati wa ufunguzi wa
kituo kipya cha Utengamao wa Watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini
Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akihutubia wananchi na wazazi, na walezi wa watoto wenye ulemavu (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto
wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...