Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake kanda ya Ziwa ya kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika shule za msingi na sekondari, maeneo ya Soko,Stendi,Minadani na maeneo mengine ya wazi ambako
wananchi walijitokeza kupata elimu sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi Bi.Gladness Kaseka amezidi kuwakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote,Kaseka alisema kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 14, 929 kati yao wajasiriamali 127,wanafunzi wa Sekondari na Shule ya msingi 3868 na wananchi 10,934.

Aliongeza pia wananchi wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko lao na kuhakikisha wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali kama nafaka,sabuni, maziwa,asali na unga lishe,juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS na kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.Kampeni hii imefanyika kwenye ngazi ya wilaya ikiwamo wilaya ya Bukoba,Kahama,Tarime na Nyamagana.

Pichani ni Mhandisi Paul Ndege kutoka TBS akitoa Elimu kwa Wafanyabiashara, wafugaji na wananchi kam walivyokutwa mnadani Tarime
Elimu juu ya Udhibiti Ubora ikiendelea kutolewa Shuleni Sirari na Mhandisi Paul Ndege wa (Afisa udhibiti Ubora TBS, Tarime.)
Sehemu ya Wajasiriamali Wa Kahama waliohudhulia semina ya Siku moja kujifunza elimu ya Udhibiti Ubora Mkoani Shinyanga.
Pichani Bwn Evarist Mrema (Kaimu Mkuu TBS Kanda ya ziwa) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza.
Pichani ni Afisa Uhusiano wa TBS Neema Mtemvu akigawa kipeperushi kwa Mkazi wa Bukoba, Mkoani Kagera mara baada ya kuelimishwa juu ya Utambuzi wa bidhaa hafifu
Pichani ni Afisa Masoko mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka akikagua bidhaa kwa mjasiliamali wa vitafunwa, maeneo ya Soko Kuu Bukoba Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...