UONGOZI wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiambatana na Serikali ya wanafunzi wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Fadhillah kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Mshauri Upendo  Mlungusye amesema wamekuwa na utaratibu wa kutembelea vituo mbalimbali vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kila mwaka mwaka.

Amesema, jamii ya chuo chao cha DUCE ni utaratibu wao ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma kwa jamii inayowazunguka na kwa mwaka huu wamechagua kutoa msaada huo kwa kituo cha Fadhillah Orphanage Group kilichopi Misugusugu Kibaha.

Upendo ameeleza kuwa kituo hicho kimekuwa na uhitaji mkubwa wa mahitaji kulingana na wingi wa watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo yenye takribani 140 kuanzia umri wa mwaka 0-14.

Mlezi wa Watoto hao, Sulekha amesema wanashukuru kwa msaada wa mahitaji mbalimbali kutoka kwa Chuo cha DUCE  na wamefurahi baada ya kuwambuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Sulekha amesema, wana watoto wadogo kuanzia mwaka 0 hadi miaka 14 na wamekuwa wanaishi nao vizuri na yeye binafsi anapenda anachokifanya cha kuwalra watoto hao.

Katibu wa Taasisi ya Fadhillah Orphanage Group Fadhil Rajab amesema wanashukuru kwa msaada huo na Kituo chao kilianza mwaka 2006 na kina jumla ya watoto 140 na wapo ambao wanasoma shule za Msingi na wengine Sekondari.

Mahitaji yaliyopelekwa kwenye kituo hicho ni mchele kg 200, Unga wa mahindi kg 120, Mafuta ya kula lt 60, Maharage kg 60, Mavazi ya aina mbalimbali, Sabuni, Madaftari na peni pamoja na Vinywaji baridi na vitafunwa mbalimbali
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE Upendo Mlungusye(wa tatu kushoto) akikabidhi mahitaji kwa Mlezi wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group Sulekha pamoja na Katibu wa Kituo hicho Fadhil Rajab walipotembelea Kituo hicho kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiongozwa na Rais wa Wanafunzi Edward Ngelewa wakikabidhi baada ya mahitaji kwa watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kutembelea kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Uongozi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na Walezi wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kutembelea kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kukabidhi mahitaji mbalimbali.
Uongozi wa Serikai ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kuwakabidhi mahitaji mbalimbali kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...