Mbunge
 wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka wanawake wa 
Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za kiuchumi na kutokubali kukatishwa 
tamaa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi ili kujijengea heshima kubwa
 katika jamii.
Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika kongamano lilioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kitengo cha Wanawake katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya MWANAMKE DUNIANI.
“Natamani kuwaona wanawake wa Dodoma mkiwa mbele kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujijengea nguvu ya kiuchumi na kujiongezea kipato.Dodoma hivi sasa baada ya tamko la Makao Makuu fursa nyingi sana zimejitokeza hivyo msilaze damu kwa kubaki kuwa waangaliaji na badala yake na ninyi mshiriki moja kwa moja”Alisema Mavunde
Akisoma Risala kwa niaba ya walimu hao kitengo “KE” Mwl Joyce Kaishozi ameeleza kwamba Chama hicho kimejipanga vyema kumjengea uwezo mwalimu mwanamke ili jamii kutambua nafasi ya Mwalimu Mwanamke na ndio maana katika kongamano walimu wamepata nafasi kupata mafunzo katika maeneo ya AFYA,*UJASIRIAMALI na UONGOZI BORA.
Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Mjumbe Wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndg Leila Burhan Ngozi na Mbunge wa Viti Maalum-Dodoma Mh Felister Bura

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...