Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SERIKALI ya Marekani imechangia Dola 500,000 kwa ajili ya kuchangia ushiriki zaidi wa wanawake kwenye mchakato wa kisiasa ambapo mchango huo utawanufaisha wanawake wa Tanzania 500 ambao watapenda kujishughulisha na mambo ya siasa.

Imefafanuliwa fedha hizo zitajumuisha mafunzo ya masuala ya kisiasa kiujumla na michakato ya uchaguzi , kutimiza malengo ya muda na jinsi ya kumudu ratiba za chama na uteuzi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Dk.Inmi Patterson wakati akizindua awamu ya pili ya mradi wa USAID/UN Women Wanawake Wanaweza wenye lengo la kuwawezesha wanawake ambapo amesema Serikali ya Marekani inachangia kulea na kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa kampeni ,jinsi ya kuandaa ujumbe, kutunga sera na kuchangisha fedha.

Amesema ukweli ni kwamba wanawake wengi wanabaki na uwakilishi hafifu kwenye michakato ya kisiasa na uchaguzi."Naamanisha ushiriki wao kama wapiga kura , wagombea na kama wawakilishi waliochaguliwa .Hii si tatizo la Tanzania pekee lakini inaonesha kwa kiasi kikubwa jinsi wanawake wanavyotengwa kwenye nafasi nyingi za juu za kufanya maamuzi kwenye Serikali Kuu na vyama vya siasa".

Amefafanua hivi karibuni iliadhimishwa Siku ya Wanawake Duniani kwa kauli mbiu ya 'Usawa Bora', kauli ambayo inaendana na mazingira ya Tanzania kwa sasa , wakati ikiongeza kasi ya maendeleo yake kuelekea kwenye viwanda na nchi zisipotilia mkazo kujenga uwezo wa wasichana na wanawake , zinasahau kuwa wanawake waliojengewa uwezo wana wanaweza kuleta mageuzi kwenye jamii.

"Sisi tunajua pale ambapo wasichana wa rika balehe na wanawake vijana wanapotunzwa vizuri inaashiria nchi iko mahali pazuri .Wao ni akina mama watarajiwa watakaoelimisha kizazi kijacho na pia ni sehemu ya injini ya baadae kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.

"Vikwazo gani vinawafanya wasichana na wanawake washindwe kuishi maisha ya kujitosheleza , vinavyosababisha kutokuwepo na usawa kwenye jamii yetu?Kwanza kabisa ni ukosefu wa elimu na ukosefu wa kupata huduma za afya.Changamoto kubwa kabisa wanawake wengi wanakosa nguvu ya kufanya maamuzi muhimu yanayohusu maisha yao na kutenda kwa uhuru bila adhabu, wasiwasi au hofu.

"Tunaweza kuona jinsi hali kama hizi zinavyoweza kujitokeza nchini Tanzania , katika baadhi ya maeneo hata ukatili wa kijinsia unahalalishwa kwa kisingizio cha utamaduni,"amesema Dk.Petterson huku akiwataka wanawake kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kijamii.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Juma Hassan amesema kuwa kupitia awamu ya kwanza ya mradi huo yeye binafsi amenufaika na mradi huo na sasa amekuwa mfano kwa wanawake wa Zanzibar.

"Kupiti mradi huu wa UN Women Wanawake Wanaweza, nimekuwa mmoja wa wanufaika kwani kupitia programu zao mbalimbali za kimafunzo nimeweza kuwa imara na kufikia malengo yangu kisiasa.Kazi ambayo ninandelea kuifanya ni kushirikiana na wanawake wa Zanzibar katika kuleta maendeleo yetu na jamii nzima kwa ujumla,"amesema.

Amesema hata katika Baraza la Wawakilishi amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake waliko ndani ya baraza hilo wanapata pia nafasi ya kuwemo kwenye kamati mbalimbali za maamuzi.

Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wawakilishi Zanzibar (WAWAZA) amesema wamekuwa na mipango mingi ya kumsaidia mwanamke wa Zanzibar na kwa sehemu kubwa wanakwenda vizuri kwani hata idadi ya wanawake inaongezeka katika nafasi za uongozi siku hadi siku.

Wakati huo huo Mbunge wa Tarime Vijijini Ester Matiku amesema kupitia mradi wa kuwawezesha wanawake kisiasa umemuwezesha hata yeye kufika hapo alipo kwani alipata nafasi ya kujengewa uwezo . "Hizi fedha ambazo zimetolewa tuwahakikishie zitatumika kwa malengo ambayo yamekusudiwa.Bnafsi nimefika hapa kwasababu ya miradi ya aina hii,"amesema Matiku.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sofia Mwakagenda ametoa shukrani kwa USAID/UN Women Wanawake Wanaweza kwani kupitia mradi wao umeibua na yeye na leo ni mbunge.Mbali ya kumuwezesha kuwa mbunge amefanikiwa kuanzisha asasi yake ambayo imesaidia wanawake 500 kwa kuwawezesha kimaendeleo na kiuchumi.
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa UN Women Wanawake Wanaweza wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi Dk.Inmi Petterson
Mbunge wa Tarime Vijijini Ester Matiko (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa kuwawezesha wanawake kupitia Usaid/Un Women wanawake Wanaweza.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Sofia Mwakagenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...