WANACHAMA na wadau wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakumbushwa kupiga simu bure ili kupata huduma kwa wakati, mwanachama anaweza akawasilisha malalamiko, maulizo na maoni.
Shirika limesema mwanachama atapiga namba ya bure 0800756773 kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 10.30 jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.
“Shirika linaendelea kuwajali,  wanachama na wadau wake, hivyo kama mwanachama akipiga namba hiyo hatopata gharama zozote za kupiga simu.” 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele, alisema kwa Upande wa NSSF  mwanachama kwanza.Tumekuja na utamaduni wa kumjali mwanachama, NSSF ipo kwa sababu ya wanachama hivyo kupata huduma ni haki yake, mwanachama anaweza akawasilisha malalamiko yake, maswali, maoni na kupata taarifa zake za michango.Pamoja na huduma ya simu mwanachama anaweza akawasiliana na Shirika kupitia barua pepe complaints@nssf.or.tz
Lulu alisema Shirika linapenda kuwahakikishia wanachama na wadau kwamba litaendelea kuboresha mifumo yake ya utendaji kazi na utoaji huduma kwa wanachama ili kuboresha na kurahisisha huduma kwa wateja.
Sehemu ya kitengo cha huduma kwa wateja



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...