Waziri wa Madini  Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd, ya  Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma. 
Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya siku tano  ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.
 Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya  uchimbaji  Mkubwa wa madini hayo. 
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko  amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria. 
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na  ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo akiwa ameambatana na Mkurungenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield wa kwanza kulia, na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo, wa kwanza kushoto ni Ali Ali, Kamishna Msaidizi Uendelezaji Migodi na Madini Wizara ya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...