*Ni yule anatuhumiwa kwa utakatishaji fedha, kumiliki majumba ya kifahari

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema itahakikisha inashirikiana na nchi nyingine ili kumpata Magreth Gonzaga aliyetoroka nchini Tanzania na kutokana na tuhuma zinazomkabili za utakatishaji fedha.

Gonzaga kwa sasa anatafutwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) ambapo mbali ya tuhuma za utakatishaji fedha anatuhumiwa kujipatia mali kupitia Kampuni ya Superior Financing Solution Limited inayodaiwa kufanya biashara bila kulipa kodi ya Serikali.

Akizungumza leo Machi 27 ,2019 jijini Dar es Salaam Wizara hiyo kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Sheria za kimataifa ambazo Tanzania nayo imesaini hakuna mhalifu anayeweza kutoroka nchini na asipatikane kwani kuna ushirikiano mkubwa kwa nchi mbalimbali duniani kusaidiana kutafuta wahalifu popote alipo.

"Ipo sheria maalumu ya kimataifa ambayo inahusika katika eneo la kusaidiana kutafuta wahalifu.Nchi yoyote ambaye mhalifu atakwenda atapatikana na kurejeshwa nchini na hivyo hivyo mhalifu akiwa wa nje nyingine kwa kukimbia chini atarudishwa nchi husika kwa utaratibu uliopo kisheria,"amesema Profesa Kabudi.

Hivyo amesema  mtuhumiwa Magreth Gonzaga atapatikana na atarejeshwa nchini na kwa sasa kinachoendelea ni kufuatilia kujua amekimbilia nchini gani na baada ya hapo Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria watachukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria na baada ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje itachukua jukumu la kumfuatilia.

Ameongeza kwa dunia hii yenye ushirikiano katika maeneo mbalimbali hakuna mhalifu anayeweza kukimbia nchini na asipatikane, hivyo Magreth ni vema akarudi nchini na kujisalimisha Takukuru  ili sheria ichukue mkondo wake.

Alipoulizwa kama tatizo na mtuhumiwa ni kutolipa kodi ya Serikali kwanini badala ya kuhangaika kutamfuta isizungumze naye alipe kodi na kisha kuachwa akaendelea na maisha yake, Waziri Kabudi amesema kinachotakiwa mtuhumiwa huyo kutafutwa na kurejeshwa nchini na kisha hatua nyingine za kisheria zifuatwe.

"Kuna dhana kuwa kosa la kutolipa kodi ni la kawaida kwa hapa nchini kwetu, ukweli kwa nchi za wenzetu ikiwemo Ujerumani kutolipa kodi ni kosa kubwa sana na ni bora uwe na kosa la kuua kuliko kulipa kodi.Kosa la kuua unaweza hata kusamehewa lakini la kutolipa kodi halina msamaha.Hivyo badala ya kukimbia nchi ni bora akarudi tu na sheria ichukue mkondo wake,"amesema Profesa Kabudi.

Jana Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athuman alitangaza kuwa wanamtafuta Magreth ambaye ametoroka nchini wakati akitambua anatafutwa kutokana na tuhuma kwa makosa mbalimbali likiwemo la utakatishaji fedha.

Magreth Gonzaga ambaye ni Mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam anatafutwa ili kujibu tuhuma za utakatishaji fedha haramu kinyume cha kifungu namba 12(d) na 13 (a) cha sheria ya utakatishaji fedha haramu ya mwaka 2006.

Hivyo Takukuru inamsaka mwanamke huyo kupitia tangazo ambalo wamelitoa kwa vyombo vya habari.Pia inaelezwa mbali ya makosa hayo , inaeleza wakati wa uchunguzi unaendelea mtuhumiwa alitoroka nchini.

Inadaiwa kwa nyakati tofauti mtuhumiwa huyo kwa kutumia fedha ambazo ni zao la ukwepaji kodi alinunua viwanja vilivyoko ufukweni mwa Bahari ya Hindi na nyumba tatu. Pia anamiliki viwanja vitatu vilivyopo Temeke jijini.

Takukuru inasema si mara ya kwanza mtuhumiwa huyo mali zake kutolewa uamuzi wa kutaifishwa ambapo katika kesi namba CC.92/2016 alikutwa na hatia  na mali zake yakiwamo magari manne na nyumba saba zenye thaman ya Sh.milioni 486 zote zilirejeshwa serikalini .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...