Na Ahmed Mahmoud Arusha

Jumuiya ya Afrika (AU) ipo katika mkakati wa kukamilisha uwepo wa soko huru la bidhaa ambapo Kwa sasa ipo kwenye mchakato wa baadhi ya bidhaa kufunguliwa Kwa zaidi ya asilimia 90 ambapo Tanzania inatarajiwa kunufaika katika soko hilo.

Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wataalamu wa biashara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mwakilishi wa wizara ya viwanda na biashara Thomas Mcharo alisema kuwa nchi hizo wanachama wataweza kuchagua bidhaa ambazo zitaweza kufunguliwa baada ya mkataba kuanza kufanyakazi ambapo Tanzania ipo njiani kuridhia mkataba huo.

Alisema kuwa uwepo wa Tanzania katika kongamano hilo ni kuona na kuufahamu zaidi mtangamano huo hivyo wakati wowote kuweza kuingia ikiwa ni faida ya nchi kwani Sera ya viwanda inaendana na masoko ya bidhaa tutakazozalisha hapa nchini

"Unajua Sera ya serikali ya awamu ya Tano ni uchumi wa Kati wa viwanda na kongamano hili tunajadili mkataba wa kubadilishana biadha katika nchi za Afrika utaona faida Kwa nchi katika kukuza biashara za bidhaa zetu"

Kwa upande wake mwakilishi wa mwenyekiti wa meza ya majadiliano ya biashara kutoka umoja wa nchi za Afrika Alexander Rubanga alisema kuwa kuondoa tozo hizo zotasaidia kukuwa Kwa biashara katika mataifa ya Afrika.

Aliziomba nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kuona umuhimu wa kuwepo makubaliano kuhusu soko la pamoja la bidhaa litakalosaidi bara la Afrika kukua kiuchumi.

Awali mtaalamu wa majadiliano kutoka time ya umoja wa Afrika Dkt.Halima Noor Abdi alisema kuwa mpaka sasa ni nchi 52 zimekwisha weka sahihi ambapo nchi zingine bado zinaendelea na majadiliano kuhusiana na umoja huo.

Amesema kuwa faida kubwa ya kujiunga na mkataba huo wa mtangamano utaidia nchi moja kuweza kuzalisha bidhaa ambazo zitaweza kuuzwa kwenye nchi nyingine barani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...