Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha


IMEELEZWA kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni changamoto kubwa  nchini Tanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla hivyo vijana wametakiwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali zenye heshima na staha.

Hayo yamebainishwa na mgeni rasmi  Father Fr.Peter wakati wa mahafali sita  ya kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari St. Mary’s Duluti amvapo ameeleza kuwa katika ulimwengu wa sasa ajira ni chache sana ukilinganisha na idadi ya watu wanaoingia katika soko la ajira.

Alibainisha kuwa ushindani katika soko la ajira ni kubwa  hivyo ni vyema Vijana wengi waliopo majumbani na mitaani kuliko kukaa  bila kazi yeyote ile wakajihusisha na shughuli za ujasilia mali zenye heshima na staha, pia wawe wabunifu

Aliongeza Vijana walio  wengi wa leo wanapenda kuwa huru(freedom) katika kufanya mambo ,Uhuru si jambo baya lakini uhuru usiokuwa na mipaka na uwajibikaji huo sio uhuru,lazima mtu awajibike kwa matendo yake mwenyewe Hivyo basi uhuru wa kweli lazima uendane na uajibikaji

Akizungumza katika mahafali hayo  Mkuu wa shule hiyo  Essau Mlengule  aliwaambia kuwa hatua waliofikia  ni kwa sababu ya bidii kubwa, nidhamu na kujituma katika  masomo mbali na hivyo pia kumtegemea Mwenyezi Mungu, akazibariki nguvu na bidii zao katika kuyatekeleza majukumu yao mema. 

Aliwataka wakaendelee kujituma, kuwa na bidii na nidhamu pindi tu warudipo  nyumbani pia wasiache hata siku moja kumtegemea Mungu katika kilajambo walifanyalo

Alisema kuwa  kuhitimu kwao kwa masomo ni   ishara ya kuwa wamekomaa kiakili, kiroho na kimwili na wapotayari kuelekea hatua mpya ya maisha kitaaluma, na maisha ya kujitegemea kiujumla.

"Ninyi kama wasomi wa kidato cha sita,  mnajukumu kubwa la kuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya maisha yenu binafsi, maendeleo ya familia,  jumuniya zenu na hatimaye maendeleo ya Taifa zima la Tanzania kwa fikra yakinifu, kwa matendo na kwa njia halali zinazokubalika na jamii ya watu walioelimika," alisema Mlengule

Alisema  mafanikio au maendeleo ya kweli hayaji kwa njia za mkato, kutokufuata taratibu za jumuiya husika, Kujichukulia maamzi bila ruhusa ya mamlaka husika,  bali  kwa kufanya kazi kwa bidii  na kwa malengo, kujiamini,  kuwa weledi (kuwa wabobezi) katika kazi zenu,  elimu ya fedha pamoja na kuwa na nidhamu ya fedha.  

Alisema Elimu yenu ya kidato cha sita iwasaidie kuwa na  ujasiri wa kuishi kwa mifano  maisha ya uadilifu katika familia na jumuiya  pia Elimu mliopata  iwasaidie kuepukana na uvivu, ulevi, uzushi, kiburi, wizi, matumizi ya madawa ya kulevya, uasherati na matendo mengine maovu yasiyokubaalika katika jamii yetu ya Tanzania kwani jamii inatarajia kuona ndani yenu maisha ya fadhila, utulivu, usikivu, uwajibikaji, ushiriki wenu katika kazi za kiuchumi na kijamii  

Alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili shule hiyo ni pamoja na upungufu Wa mabweni ,ukosefu Wa jengo la utawala pamoja na viwanja vya michezo.
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...