Hakimu wa mahakama ya Mwanzo, Maromboso iliyopo jijini Arusha,Therezia Sidoyeka amejikuta katika wakati mgumu Mara baada ya karatasi za hukumu aliyokuwa alisome mahakamani kutoweka katika mazingira ya utata na kusababisha ashindwe kutoa maamuzi ya mahakama katika shauri la mirathi ,lililopo mbele yake.
"Jamani hukumu yenu niliyokuwa nimeiandaa kwa kuichapa imetoweka hata sijui ilipo inaonekana baadhi yenu mnaomba sana ,naombeni niandae upya ili niisome jumatatu itakuwa tayari" Alisema hakimu Sidoyeka.
Tukio hilo lisilo la kawaida limetokea mwishoni mwa wiki katika mahakama hiyo na kufanya baadhi yabwasikilizaji kupigwa na butwaa.
Shauri la kesi hiyo Namba 109 la mwaka 1992 lililetwa mahakamani hapo na mlalamikaji , Stephano Balthazar akimpinga Frida Swai ambaye ni mama yake mdogo kuwa msimamizi wa Mirathi ya Marehemu bibi yake aitwaye Monica Mbowe, aliyefariki mwaka 1992 kwa madai ya kushindwa kukusanya,kugawa na kufunga Mirathi katika kipindi cha miaka 28.
Kupotea kwa karatasi za hukumu hiyo kumeibua sintofahamu katika maamuzi ya mahakama hiyo huku upande wa waleta maombi wakijawa na hofu zaidi ,ukizingatia kuwa nyumba moja ya marehemu iliuzwa kwa Jaji Mstaafu Aishiel Sumari.
Shauri hilo limeahirishwa kwa Mara ya pili mfululizo bila kuwepo na sababu za msingi,ambapo aprili 30,mwaka huu shauri hilo lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi hata hivyo hakimu Sidoyeka hakuwepo mahakamani hapo na kuelezwa kuwa shauri hilo limepangiwa tarehe ya Leo,Mei 3 mwaka huu.
Leo wasikilizaji wa pande zote mbili katika shauri hilo walifurika katika chumba cha mahakama huku kila upande ukiwa na shauku ya kutaka kujua maamuzi yatakayotolewa mahakama hapo.
Awali shauri hilo lilianza kuunguruma mahakamani hapo, April 11 mwaka huu,ambapo upande wa mleta maombi ,Stephano Balthazari akiwa na mashahidi sita, alimpinga msimamizi wa Mirathi Frida Swai kwa madai si mwaminifu,ameshindwa kukusanya Mali za Marehemu na kugawa katika kipindi cha miaka 28 tangu kifo cha marehemu.
Pia alidai kuwa anaoushahidi kuwa Frida Swai amefuja Mali za marehemu bibi yake kwa kuuza baadhi ya nyumba zilizoashwa ikiwemo nyumba ya Kaloleni (Mviringo bar)ambayo ameiuza kwa Jaji Mstaafu Aishiel Sumari bila kufuata taratibu.
Upande wa mjibu Maombi ,Frida Swai aliyekuwa na mashahidi wanne aliiambia mahakama hiyo kwamba Aligawa Mirathi ya marehemu Monica Mbowe mwaka 1995 kwa kufuata wosia wa marehemu ulivyoelekeza.
Alisema kuwa marehemu aliacha Nyumba sita zikiwemo NNE zilizopo Ungalimited na Mbili zipo kaloleni jijini hapa ambapo Nyumba tatu aligawa moja kwa mjukuu mmoja ,moja kwa Mtoto pekee wa marehemu na nyingine kwa rafiki wa marehemu huku yeye akijigawia Nyumba tatu.
Shauri hilo limepangwa kutolewa uamuzi Mei 6 mwaka huu siku ya jumatatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...