Na Ahmed Mahmoue,Longido

Mbunge wa Longido Stevin Kiruswa,amemtaka Mwenyekiti wa Kijiji cha Eworndeke katika kata ya Kimokokuwa,Mosses Leng'ese kurejesha haraka kiasi cha sh,milion 69 kati ya Mil.135 alizopokea kinyume cha sheria kupitia mradi wa umeme wa grid ya Taifa ili zitumike kuwasaidia akina mama wa kifugaji kama ilivyoamriwa na wananchi wa Kijiji hicho.

Kiruswa ametoa kauli hiyo jana kijijini hapo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliolenga kupata ufumbuzi juu ya fedha za Kijiji zinazodaiwa kutafunwa na mwenyekiti wa Kijiji hicho Mosses Leng'ese na wenzake sita.

Awali mwenyekiti wa Kijiji hicho,Leng'ese na wenzake walidaiwa kujimilikisha maeneo ya wazi ambayo ni Mali ya Kijiji na kujipatia kiasi cha sh,milioni 135 jambo lililoibua mgogoro mkubwa ambao ulimlazimu mkuu wa wilaya Frank Mwaisumbe kuingilia kati na kumtaka mwenyekiti huyo kurejesha sh,milioni 69 kwa wananchi.

Aidha mbunge huyo aliwataka wananchi kuachana na migogoro isiyo na tija badala yake wajielekeze katika utatuzi wa changamoto ikiwemo kuwekeza kwenye ujenzi wa madarasa kwa kuwa suala la ufugaji limekuwa na changamoto ya mifugo kufa kutokana na hali ya ukame.

Naye wakili wa kujitegemea ambaye ni Mzaliwa wa kijiji hicho na mkazi wa Kijiji Arusha,Nicolaus Senteu,alisema mkutano huo umeafikiana kumsamehe mwenyekiti huyo na wenzake kwa sharti la kurejesha fedha hizo na kwamba hatua hiyo imeleta afya kwa Kijiji hicho kuepusha mfarakano.

Aliipongeza jamii hiyo kwa kuonyesha msimamo wa kupigania rasilimali yao iliyotaka kutumika vibaya na wajanja wachache ili itumike kwa manufaa ya wananchi wote.

"Nawashukuru wananchi wa Eworndeke kwa kuonyesha msimamo hasa pale wanapoona rasilimali yao inataka kuporwa na watu wachache kuweza kuirejesha" Alisema Senteu

Aliwashauri viongozi wa Kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wananchi kwa uwazi zaidi suala litakalosaidia kuondoa migongano ya kimaslahi na kuleta umoja na mshikamano.

Katika hatua nyingine wananchi hao wametaka kiasi cha sh,million 700 zinazotarajia kulipwa kama fidia ya maeneo ya wazi ya kijiji ili kupisha mradi wa umeme wa Grid ya Taifa KV 400 ,zilipwe kupitia akaunti ya kijiji na zitumike ipasavyo kuwaletea maendeleo wananchi.

Wananchi hao walikubaliana kwamba kati ya fedha hizo,sh, milioni 400 zigawanywe kwa vitongoji vinne vya Kijiji hicho na kiasi cha shilingi milioni 300 zitumike kuibua maendeleo Kijiji hapo ikiwemo ujenzi wa madarasa na zahanati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...