Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba,amewataka watumishi wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC) kuhakikisha wanafanya kazi ya msako ya mifuko ya plastiki mpaka siku za mapumziko ili kuondokana na mifuko hiyo.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati uzinduzi wa sheria ya katazo ya sheria ya mifuko ya plastiki iliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam amesema hakuna kulala kwani kazi ya utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki ndio imeanza Juni Moja.

Katika utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki Waziri Makamba alifanya ziara ya ukaguzi kwenye soko la kariakoo kuangalia utekelezaji wa agizo la kuanzia leo tarehe moja mwezi wa sita la kutotumia mifuko ya plasticki kwa lengo la kulinda mazingira na afya za wananchi kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya makubwa mifuko ya plastiki.

Amesema katika utekelezaji wa agizo hilo ni wakati wa bodi ya NEMC kuhakikisha wafanya kazi ambao wapo kwenye kikosi kazi cha kukagua watumiaji wa mifuko hiyo iliyokatazwa kufanya kazi kwa kasi zaidi ikiwemo kufanya kazi mpaka siku za mapumziko.

"Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa sheria hii mpya ni wakati wa bodi ya Nemc kuwataka wafanya kazi waliopewa kufanya kazi ya ukaguzi wa mifuko kufanya kazi mpaka siku ya mapumziko kuhakikisha mifuko hii inapotea."amesema Makamba.

Makamba amesema nchi haijakurupuka Kaukataza matumizi ya mifuko ya plastiki baada ya kubaini mifuko hiyo ibaharibu mazingira ambapo akitoa mfano endapo Tanzania ikiendelea na matumizi ya mifuko hiyo katika kipindi cha miaka 20 ijayo Baharini kutakuwa na mifuko mingi kuzidi samaki jambo analodai ni hatari kwa mazingira.

Hata hivyo, Waziri Makamba amesema shehena ya mifuko ya plastiki iliyopatikana kutoka kwa watumiaji itapelekwa kutengenezea Bomba na madawati hivyo akiwasihi wananchi kusalimisha ya plastiski kwenye mamlaka husika .

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya ya NEMC,Profesa Esnati Osinde amesema watataendelea kutoa elimu hadi kwa viongozi wa dini kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba akizungumza na watendaji  wa  Baraza la Taifa la Uhifadhi wa  Mazingira (NEMC) katika utekelezaji wa Sheria ya uzuiaji wa mifuko ya plastiki katika soko la Kariakoo
 Mifuko mbadala ambayo wanatakiwa kutumia wananchi katika Kubebea bidhaa mbalimbali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira Dkt. Samwel Gwamaka akitoa mikakati ya Baraza katika utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki.
 Wajasiriamali wakionesha vibebesheo mbalimbali katika uzinduzi wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki  iliyofanyika mbagala jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba akizungumza wakati uzinduzi wa sheria katazo ya mifuko ya plastiki iliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
 Vibebesheo mbalimbali ambavyo vinatakiwa kutumika ubebaji wa bidhaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na January Makamba akiangalia mfuko mbadala baada  ya kuanza sheria ya katazo la mifuko  plastiki  katika operesheni iliyofanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...