Na Ripota Wetu,Wa Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ameapa kupambana na wanaotorosha Dhahabu na mpaka sasa na watu wawili wametiwa Mbaroni kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria .
Homera ameyasema hayo mkoani Katavi akiwa katika ziara ya kutembelea migodi mbalimbali ukiwemo wa Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.
Amesema anachotaka nikuona wachimbaji wadogo wanauza madini yao katika soko la madini lililopo mkoa huo .
Homera ameanza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa tayari soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu Gram 238, Mei 23 mwaka huu wa 2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa hali iliyonayosababisha soko hilo kusua sua.
Amesema kutokana na hali hiyo bosi huyo wa mkoa alimua kufanya ziara ambayo ilikwenda kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo ambapo hadi sasa linaridhisha na kufuatia oparesheni mbalimbali zinazoendelea Soko linaendelea kufanyika kwa ununuzi na uuzaji wa madini na mpaka sasa Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Sh. 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na Juni 30/2019 na Serikali kupata mrahaba (Royality7%) Sh. 36,340,858.92 na Service levy asilimia 0.3 sawa na Sh.1,401,718.85,
Pia amefafanua kuwa ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo nakwamba ameendelea kuwa bana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili kujenga uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi kwa kulipa kodi.
Wachimbaji wadogo wadogo wakimsikiliza MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa katika ziara ya kutembelea migodi mbalimbali ukiwemo wa Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.
MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa katia ziara ya kutembelea migodi mbalimbali ukiwemo wa Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...