Habari za Leo,
Pole na majukumu ya siku nzima.
Napenda kukujulisha kuwa ndugu Salum Ramadhan Salumu (18) ,BADO hajapatikana wala hatujapata taarifa zake.
Tafadhali naomba msaada wako wa kila njia (Instagram,Facebook, Twitter,Radio,TV,Blog,Makundi ya WhatsApp,Website Nakadhalika) kusambaza taarifa ya Kupotea kwa kijana Salum Ramadhan Salum (18) ambaye hakurejea nyumbani tangu tarehe 12th May 2019. Mara ya mwisho ameonekana stendi ya Ukonga madafu akipanda gari ya kutoka Gongo la Mboto likielekea buguruni ikiwa ni safari yake ya kurejea nyumbani majira ya saa 2 usiku.
Alikuwa amevaa shati jeupe na Suruali ya kijivu na saa rangi ya dhahabu na sendoz za wazi. Tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu na wewe au naomba unijulishe kwa kupiga ama kuandika sms kwenda nda namba 0713/0766-202748.
Ni kijana mpole na mwenyeji wa Kiwalani BomBom kwa DSM na Mwanza ndio alipozaliwa.
Naaomba Ushirikiano wenu kwenye changamoto hii.
Asante
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...